John 18

1Baada ya Yesu kusema maneno haya, aliondoka na wanafunzi wake kuelekea bonde la Kidron, ambako kulikuwa na bustani, ambako yeye na wanafunzi wake wakaingia ndani yake. 2Sasa yule Yuda, aliyetaka kumsaliti, naye alilijua eneo hilo, kwani Yesu alikuwa akienda hili eneo mara kadhaa akiwa na wanafunzi wake. 3Naye Yuda, baada ya kuwa amepata kundi la maaskari na maofisa toka kwa wakuu wa makuhani, wakaja wakiwa na taa, kurunzi na silaha.

4Naye Yesu, hali akijua kila kitu kilichokuwa kikifanyika dhidi yake, alijitokeza mbele na akawauliza, “Ni nani mnayemtafuta?” 5Nao wakamjibu, “Yesu Mnazareth.” Yesu akawaambia, “Mimi ndiye” Naye Yuda aliyemsaliti, alikuwa amesimama pamoja na wale askari.

6Kwa hiyo alipowaambia, “Mimi ndiye” walirudi kinyume na kuanguka chini. 7Halafu akawauliza tena, “Ni nani mnayemtafuta? Nao wakamjibu tena “Yesu mnazareth.”

8Yesu akawajibu, “Nimekwisha kuwaambia kuwa Mimi ndiye; kwa hiyo kama mnanitafuta mimi, waacheni hawa wengine waende.” 9Haya yalikuwa hivyo ili lile neno litimilike; pale aliposema; “Katika wale ulionipa, sikumpoteza hata mmoja.”

10Ndipo Simon Petro, aliyekuwa na upanga, akaufuta na kumkata sikio la kulia mtumishi wa Kuhani mkuu. Na jina lake mtumishi yule lilikuwa Malko. 11Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako kwenye ala yake. Kwa nini nisikinywee kikombe kile alichonipa Baba?”

12Basi lile kundi la askari na jemedari, na watumishi wa Wayahudi, walimkamata Yesu na kumfunga. 13Nao wakamwongoza kwanza mpaka kwa Anasi, kwani yeye alikuwa mkwe wa Kayafa, ambaye ndiye aliyekuwa Kuhani mkuu kwa mwaka huo. 14Sasa Kayafa ndiye aliyekuwa amewapa ushauri Wayahudi ya kwamba ilimpasa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.

15Simon Petro alimfuata Yesu, na vivyo hivyo mwanafunzi mwingine. Na yule mwanafunzi alikuwa akifahamika kwa kuhani mkuu, naye akaingia pamoja na Yesu katika behewa ya Kuhani mkuu; 16lakini Petro alikuwa amesimama nje ya mlango. Basi yule mwanafunzi aliyekuwa akifahamika kwa kuhani mkuu, alitoka nje akaenda kuongea na yule mwanamke mtumishi aliyekuwa akilinda mlango na kumwingiza Petro ndani.

17Basi yule kijakazi aliyekuwa akilinda mlango, alimwambia Petro, “Je wewe si mmoja wa wafuasi wa huyu mtu?” Naye akasema, “Mimi siye.” 18Na wale watumishi na wakuu walikuwa wakisimama mahali pale; wamekoka moto wa kwa maana, kulikuwa na baridi, na hivyo walikuwa wakiota moto ili kupata joto. Naye Petro alikuwa nao, akiota moto akiwa amesimama.

19Kuhani mkuu alimhoji Yesu juu ya wanafunzi wake na mafundisho yake. 20Yesu akamjbu, “Nimeuambia waziwazi ulimwengu; Mimi nilifundisha mara kwa mara kwenye masinagogi na hekaluni mahali ambapo wayahudi hukusanyika. Nami sikusema lolote katika siri. 21Kwa nini mliniuliza? Waulizeni walionisikiliza juu ya kile nilichosema. Hawa watu wanajua mambo yale niliyosema.

22Yesu alipokwisha sema hivyo, mmoja wa wakuu aliyekuwa amesimama akampiga Yesu kwa mkono wake na kisha akasema, “Je, hivyo ndivyo inavyokupasa kumjibu kuhani mkuu?” 23Naye Yesu akamjibu, “Kama nimesema jambo lolote baya basi uwe shahidi kwa ajili ya uovu, na kama nimemjibu vyema kwa nini kunipiga? 24Ndipo Anasi alipompeleka Yesu kwa Kayafa kuhani mkuu akiwa amefungwa.

25Sasa Simoni Petro alikuwa amesimama akijipasha joto mwenyewe. Halafu wale watu wakamwambia. “Je, wewe pia si mmoja wa wanaafunzi wake?” Akakana akisema “Mimi siye.” 26Mmoja wa watumishi wa kuhani mkuu, ambaye alikuwa ndugu wa yule mwanaume ambaye Petro alimkata sikio, alisema, “Je si wewe niliyekuona naye kule bustanini?” 27Petro akakana tena, na mara Jogoo akawika.

28Kisha wakamchukua Yesu toka kwa Kayafa mpaka kwenye Praitorio. Ilikwa asubuhi na mapema. Wao wenyewe hawakuiingia ile Praitorio ili wasije wakanajisika na kuila pasaka. 29Kwa hiyo Pilato akawaendea akisema. “Ni shitaka gani linalomhusu huyu mtu?” 30Wakamjibu na kumwambia, “Kama huyu mtu asingekuwa mtenda maovu, tusingemleta kwako.”

31Pilato akawaambia, “Mchukueni ninyi wenyewe, mkamhukumu kulingana na sheria yenu.” Nao Wayahudi wakamwambia, “Sheria haituruhusu sisi kumwua mtu yeyote.” 32Walisema haya ili neno la Yesu litimilike, neno ambalo alikuwa amekwisha sema juu ya aina ya kifo chake.

33Basi Pilato akaingia tena Praitorio akumwita Yesu; akamwambia, “Je, wewe ni mfalme wa Wayahudi?” 34Yesu akamjibu, “Je, wewe waniuliza swali hili kwa Sababu wataka kujua au kwa sababu wengine wamekutuma ili uniulize mimi?” 35Naye Pilato akamjibu, “Mimi si Myahudi, au sivyo?” Taifa lako na kuhani mkuu ndio waliokuleta kwangu; wewe umefanya nini?

36Yesu akajibu; “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu, kama ufalme wangu ungekuwa na sehemu katika ulimwengu huu watumwa wangu wangenipigania ili nisitolewe kwa wayahudi. Kwa kweli ufalme wangu hautoki hapa” Basi 37Pilato akamwambia, “Je, wewe basi u mfalme?” Yesu akajibu, “wewe ndivyo unanvyosema kuwa mimi ni mfalme, Kwa sababu hii mimi nilizaliwa na kwa sababu hii mimi nimekuja ulimwenguni ili niwe shahidi wa ile kweli. Yeyote aliye wa hiyo kweli huisikiliza sauti yangu.

38Pilato akamwambia, “Kweli ni nini?” Naye alipokwisha sema haya akaenda kwa Wayahudi na kuwaambia “Siona katika lolote mtu huyu. 39Ninyi mna utamaduni unaonifanya nimfunfungulie mfungwa mmoja wakati wa Pasaka. Je mnataka nimfungulie mfalme wa Wayahudi.” Kisha walipiga kelele wakisema, siyo huyu, tufungulie Baraba.” Naye Baraba alikuwa mnyang’anyi.

40

Copyright information for SwaULB